Huduma ya kukoboa Nafaka
Tuna huduma za kukoboa mpunga kwa zaidi ya tani 10 kwa siku,kutenganisha mchele kulingana na ukubwa wa punje zake,kung’arisha na pia kupakia mchele huo kwenye mifuko bora ya ujazo tofauti kulingana na mahitaji.
Kituo cha Madawa ya Mifugo na mazao
Kituo chetu kinatoa huduma za dawa kwa mazao mbalimbali, ndege na wanyama wote wa kufugwa. Pia tunafanya uchunguzi wa kimaabara ili kupata suluhu mbalimbali za matatizo mbalimbali yanayoathiri mimea na wanyama.
HUDUMA ZETU ZIJAZO
Duka la dawa
Tuna mpango wa kuanzisha duka la dawa za binadamu ili kutoa huduma za dawa na ushauri juu ya masuala mbalimbali ya afya kwa jamii inayotuzunguka. Tunaamini kuwa tutaweza kuwa na uhusiano wa kushauriana na wateja wetu, huku tukielewa umuhimu wa maadili, usiri, uhuru wa mgonjwa na kuwa tegemezi.
Duka la Nyama
Tunatarajia kuwa na duka la nyama lenye vifaa vya kisasa vya uchinjaji, wataalam wa kuwachinja wanyama kulingana na mahitaji ya mteja. Pia tutaitundika nyama kwenye kibaridi chetu kwa muda unaohitajika au tutachinja mnyama tayari kwa kufungashwa na kuwekwa lebo ikihitajika. Tutatengeneza bidhaa zetu za Kuku na Soseji. Wateja watakuwa huru kutupigia simu ilikujadili chaguo tofauti za usindikaji