Ujumbe wa Waanzilishi
J&J Agricultural Company Limited
Mpendwa Mheshimiwa Mteja na Mgeni kwenye Tovuti yetu,
Wewe hukuzaliwa kwa bahati mbaya, wala wewe hukutokea kama ajali. Hata kabla ya Ulimwengu kuumbwa, Mungu alikuwa anakufikiria, na alipanga hatma yako kwa makusudi yake. Sisi waanzilishi wa Kampuni ya Kilimo iitwayo J &J Agricultural Company Limited, tukiwa Watanzania wazawa na wazalendo wenye uthubutu, tunajivunia ninyi nyote.
J&J Agricultural Company Limited inafuraha kukukaribisha kwenye Tovuti yetu ambayo huonyesha aina tofauti za maudhui kila wakatimtumiaji anapoitazama (dynamic),ambayo utapata manufaa kwa biashara zako na kukuwezesha kutosheleza mahitaji yako.
Sote wawili (James na Joyce)ni Mwana na Binti wa wazazi wakulima wadogo na kwa hivyo ukulima (damu yetu) umekuwa ndoto yetu tangu siku tulipooana. Ili kutekeleza Dira/ndoto yetu ipasavyo, huku tukitambua kuwa ni watu ndio wanaofanya mambo yatendeke na kufanya kazi kwa kuelekea ukuaji na maendeleo ya wengine, tuliamua kuanzisha kampuni binafsi ya kiwango cha kati ambayo ilianzishwa na kusajiliwa nchini Tanzania mnamo Oktoba 2019.
Wazo la awali la kampuni yetu lilikuwa kujihusisha na kilimo mchanganyiko kitegemeacho mvua, pamoja na ufugaji wa aina mbalimbali za mifugo na kuku.
Sera ya Serikali ya kukuza sekta binafsi na ukombozi wa biashara na uwekezaji imetoa mazingira ya kuvutia na yanayofaa kwa shughuli za biashara ndogo ndogo, na hivyo kuibua fursa za ukuaji wa soko usio na kifani, hasa katika kilimo.
Kama waanzilishina wamiiki wa Kampuni, tunaamini kuwa mtaji mkuu wa maendeleo ya biashara ni akili na maarifa. Tumedhamiria kufanya kadri tuwezavyo, kuchangia juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongeza ajira, kufikia Malengo ya Milenia ya Dunia na kutimiza malengo ya Dira ya Tanzania 2025, hususanikatika utekelezaji kwa vitendo wa Sera ya Viwanda na Uzalishaji.
Katika mazingira hayo, J&J Agricultural Company Limited ililazimika kuimarisha nguvu yake ya kilimo-biashara kwa kuendelea kupanua ekari za kilimo kupitia upatikanaji wa ardhi zaidi na uendelezaji wa vifaa, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mabwawa yaasili na mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji, ufugaji wa samaki na ufugaji wa aina mbali mbali za mifugo.
Shughuli hizo ni pamoja na kilimo na upandaji wa mpunga, mahindi, dengu, mboga mboga, matunda (ndizi, matikiti maji, embe, limao, mapapai, michungwa,n.k) kupitia skimu za umwagiliaji na kuongeza mifugo. Tumeanzisha miradi ya ufugaji samaki kwenye mabwawa na vizimba. Pia tunafuga ng’ombe wa maziwa na nyama, mbuzi, kondoo, kuku, batabukini, bata mzinga na nguruwe.
Shamba hilo lipo katika kijiji cha Kitomondo, bonde la Ruvu, Wilaya ya Kibaha Vijijini, mkoani Pwani, kilometa 70 kutoka jijini Dar es Salaam, barabara kuu ya Morogoro, na kuchepukiakushoto paleMlandizi, ambako kampuni ina ofisi zake kuu.
Mitambo mitatu ya kisasa imesimikwa Mlandizi;mmoja wa usindikaji wa mpunga, kuweka daraja(grading) na kufungasha mchele. Mingine miwili ina kazi tatu za usindikaji wa chakula tofauti cha mifugo, samaki na kuku(pellets).
Tumeonesha kwenye Tovuti yetu hii jinsi tunavyoongeza thamani ya huduma na bidhaa zetu, kwa kutengeneza bidhaa za maziwa, nyama, mchele, na vyakula mbalimbali vya mifugo. Mbolea, pembejeo za kilimo, pamoja nanafaka za kila aina pia zinaoneshwa.
Uzoefu unaonyesha kwamba aina hii ya biashara katika viwango vidogo na vya kati haihitaji idadi kubwa ya wafanyakazi wa kudumu. Hata hivyo, J&J Agricultural Company Limited inalenga ..
utendakazi wa hali ya juu wa Kampuni utakaotokana nautendakazi wa hali ya juu wa mtu binafsi katikaKampuni.Tunahakikisha kuwa kuna idadi na aina sahihi ya watu katika maeneo sahihi na kwa wakati unaofaa, wenye uwezo wa kutoa mawazona kutekeleza kwa vitendo na vema kazi wanazokabidhiwa.
Mwandishi na mhamasishaji Simon Sinek aliwahi kusema: ‘Kiongoziasiye na cheo ni bora kuliko akiwa na cheo bila uwezo wa kuongoza’. Kwa kukubaliana naye, tunathamini juhudi na utendakazi wa kibunifu wa mtu binafsi (na si cheo chake) na kutoa ushauri wa asili kupitia mawazo ya kimkakati kama msingi wa mipango ya waajiriwandani ya Kampuni.
Tunaamini katika ubunifu, uvumbuzi na kukumbatia fursa zinazopatikana nchini kwa kushiriki katika kuanzisha miradi jumuishi katika nyanja zinazotuvutia.
Dira/ndotoyetu ni kuwa Mjasiliamali Mkubwa mwenye biashara kubwa zenye kuaminiwa (Anza Kidogo na kisha Ukue zaidi)’ikiwezeshwa na Dhamira/Dhima/Utume usemao ‘kuwafanya wateja wetu wajisikie furaha zaidi kwa kuwapatia bidhaa bora, na Mashamba ya Maonyesho (Kilimo Darasa)’.
Kumbuka: ukichagua kusafiri kwenye ziwa la Bidhaa Bora na Biashara, jenga kampuni yako kama ambavyo ungejenga mashua yako, yenye nguvu ya kusafiri kwa usalama bila kujali dhoruba yoyote. Tumefanya hivyo kupitia kurahisisha jinsi kazi inavyofanywa, na kuwa na muda zaidi wa kupata faida kubwa zaidi: hiyo ni kutoka ugumu wa mifumo mchanganyiko ya kiuendeshaji hadi urahisisho wake.
Kwa kumalizia, tunawaomba wadau wetu wote; ndugu na dada zetu kutuunga mkono kwa kufanya kazi nasi kwa njia moja au nyingine. Tunahitaji wanunuzi na wauzaji wa malighafi, taasisi za fedha, wauzaji wa jumla wa mashine na vipuri ili kwa pamoja tusaidiane kutengeneza mnyororo utakaotuunganisha sotena soko la ndani na nje, taasisi za fedha na wauzaji reja reja, jumla na wanunuzi wa kimataifa. Tunasubiri kwa hamu kusikia kutoka kwako.
Kwa mara nyingine tena, tunatanguliza shukurani zetu kwa kutembelea Tovuti hii, na tunakuomba ujaribu huduma na bidhaa zetu.
Mungu akubariki sana.