Ghala Namba 1
Hili ni ghala letu kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya magunia elfu tatu ya mazao/nafaka. Ghala liko Mlandizi ilipo makao makuu ya Kampuni, lina hewa ya kutosha na halipati jua la moja kwa moja.
Ghala Namba 2
Hili pia liko katika majengo yetu ya kiwanda pale Mlandizi na hutumika kwa ajili ya kuweka mchele baada ya kukobolewa, kutenganishwa na kufungashwa. Ghala lina hewa ya kutosha na halipati jua la moja kwa moja.
Ghala Namba 3
Ghala hili pia liko katika majengo yetu ya kiwanda pale Mlandizi. Lina mashine zinazosindika vyakula vya mifugo aina zote (wanyama, ndege na samaki. Kwa sababu ya ukubwa wake, kazi yake ni kuhifadhi malighafi, lakini pia hutumika kama sehemu ya kusindikia na kuhifadhi vyakula vya mifugo, kuku na samaki
vilivyosindikwa.
Ghala Namba 4
Kampuni imepangishwa ghala kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi hadi tani mia tatu za nafaka mbali mbali. Ghala hili liko Mbagala Rangi Tatu, Wilayani Temeke. Ghala hili pia lina hewa ya kutosha na halipati jua la moja kwa moja.
Ghala Namba 5
Hili ni ghala jipya kabisa ambalo Kampuni imelijenga katika eneo la Mbwade (Ndutumi) Wilaya ya Morogoro Vijijini. Ghala lina uwezo wa kuhifadhi hadi tani mia tano za nafaka mbali mbali. Ghala hili pia lina hewa ya kutosha na halipati jua la moja kwa moja. Ghala letu hili linaweza kutumiwa na mtu yeyote kwa
maelewano ya kibiashara.
MAGHALA YETU YAJAYO
Ghala Namba 6
Kampuni ina eneo kubwa pale Dumila Mkoani Morogoro na inatarajia kujenga ghala kubwa zaidi la kisasa lenye uwezo wa kuhifadhi hadi tani elfu moja za nafaka mbali mbali. Ghala hili pia litakuwa na hewa ya kutosha na halitapata jua la moja kwa moja.