Huduma ya kukoboa Nafaka
Tuna huduma za kukoboa mpunga kwa zaidi ya tani 10 kwa siku,kutenganisha mchele kulingana na ukubwa wa punje zake,kung’arisha na pia kupakia mchele huo kwenye mifuko bora ya ujazo tofauti kulingana na mahitaji.
J & J Agricultural Company Limited ni Kampuni ya Kibinafsi ya Wastani, iliyoanzishwa na kusajiliwa nchini Tanzania mwezi Oktoba 2019 chini ya Sheria ya Makampuni (Sura ya 212) ikiwa na Cheti cha Ushirika Na. 140114502.
Soma zaidiDira yetu ni kuwa Mjasiliamali Mkubwa mwenye biashara kubwa zenye kuaminiwa.
Dhamira yetu ni kuwafanya wateja wetu wajisikie furaha zaidi kwa kuwapatia bidhaa/huduma bora na kuwa na Mashamba ya Maonyesho (Kilimo Darasa).
Malengo ya Kampuni ni ya aina mbili: Kwanza, ni kutoa huduma bora kwa wateja katika uwanja wa kilimo, ufugaji, usindikaji mazao ili kuongeza thamani, kuuza bidhaa tunazozalisha na kutoa ushauri katika maeneo hayo; Pili, kuwa na shughuli kubwa za biashara inayozalisha faida kubwa
Tunaamini katika ubunifu, uvumbuzi na kukumbatia fursa nyingi zinazopatikana nchini kwa kushiriki katika kuanzisha miradi jumuishi katika nyanja zinazotuvutia.
Tunatengeneza vyakula vya mifugo kwa wanyama na ndege kama vile ng'ombe, kuku na nguruwe. Tunatambua vyakula vya mifugo kama nyenzo muhimu kwa wafugaji, na kwa sababu hiyo, viwango na taratibu zilizofafanuliwa na programu yetu ya uhakikisho wa ubora (quality assurance) zinawekwa.Aidha, tunatengeneza pia vyakula vya samaki kuanzia vifaranga hadi vile vya kuelea kwa ajili ya samaki wakubwa.
Bidhaa zinazotokana na kilimo cha bustani, ambazo ni pamoja na matunda kama vile maembe, tikitimaji, ndizi, mapapai, malimau na maparachichi zinapatikana shambani na katika maduka yetu husika. Pia tunatoa mboga kama vile mchicha, tembele, nyanya na pilipili za kijani, njano na nyekundu.
Nafaka kama vile mchele, soya, maharage, alizeti, mtama na ufuta zinazopatikana katika orodha yetu zinauzwa. Nafaka nzima (whole grain) ikiwa ni kiungo cha chaguo la kwanza la wengi, nafaka zetu ni nzuri kwa kutumika kama chaguo la mlo wa gharama ya chini kwa wateja wanaotafuta vyakula vitamu na lishe siku nzima.